ResearchBib Share Your Research, Maximize Your Social Impacts
Sign for Notice Everyday Sign up >> Login

MIELEKEO YA WANAFUNZI WA KIDATO CHA TATU NA CHA NNE KUHUSU METHALI KINZANI: UCHUNGUZI KATIKA SHULE ZA UPILI KATIKA KATA YA TOWNSHIP, KAUNTI YA KITUI; KENYA

Journal: International Journal of Advanced Research (Vol.6, No. 10)

Publication Date:

Authors : ;

Page : 1374-1381

Keywords : Ukinzani Methali za Kiswahili mtumiaji lugha Jozi za methali Mwelekeo;

Source : Downloadexternal Find it from : Google Scholarexternal

Abstract

Ukinzani ni dhana ambayo imefasiliwa kama ubishi au upinzani. Ukinzani katika methali za Kiswahili unaweza kufasiliwa kama unyume wa kimaana unaoletwa na methali ambazo ziko katika jozi moja na zinazotoa maana zilizo kinyume. Methali za Kiswahili zina maana na ili maana hiyo ijitokeze kwa namna inayofaa, kila methali inapaswa kutumika katika mazingira yanayooana na maana ya methali mahususi. Methali zina jukumu la kuonya, kusifu, kukashifu, kuelekeza, kuliwaza na kadhalika. Aidha, katika fasihi ya Kiswahili kuna jozi za methali zilizo na maana kinyume. Kwamba, methali moja inakuelekeza huku na nyingine inakupa mwelekeo unaotofautina na ule wa awali. Katika hali kama hii, mtumiaji lugha na mwanajamii kwa jumla anaweza kupatwa na utata wa mwelekeo atakaoufuata. Methali zinapotoa maana zinazopingana basi utata unaweza kujitokeza haswa ukimsemea nwanajamii methali kisha naye akutajia iliyo na maana kinyume, huenda suluhu ya mnachozungumzia ikakosekana. Hali hii ndiyo ilimsukuma mtafiti akitaka kubainisha namna wanajamii wanavyochukulia kuwepo kwa ubishi katika methali za Kiswahili, ikizingatiwa kwamba methali hizi hutumika kila mara na wanajamii katika mazungumzo, nyimbo na hata katika uandishi.

Last modified: 2018-11-14 21:00:30