ResearchBib Share Your Research, Maximize Your Social Impacts
Sign for Notice Everyday Sign up >> Login

UREJELEOMATINI KATIKA UWASILISHAJI WA MAUDHUI YA DHULUMA KATIKA RIWAYA YA MSICHANA WA MBALAMWEZI (K.W.WAMITILA)

Journal: International Journal of Advanced Research (Vol.7, No. 5)

Publication Date:

Authors : ; ;

Page : 303-308

Keywords : Urejeleomatini riwaya za kimajaribio mbinu za kimajaribio.;

Source : Downloadexternal Find it from : Google Scholarexternal

Abstract

Waandishi wa riwaya ya Kiswahili ya kisasa wanawasilisha ujumbe kwa hadhira kwa kujikita katika mbinu za kiuandishi za kimajaribio. Urejeleomatini ni mojawapo wa vipengele muhimu vya mbinu hizo za kimajaribio. Riwaya zenyewe zimeitwa ?riwaya za kimajaribio? au ?riwaya za kisasa?. Watalaamu wengine wamezibaini kama ?riwaya za Karne ya Ishirini na Moja. Mwandishi Kyallo Wadi Wamitila ni mmojawapo wa waandishi wa kisasa anayetumia mtindo huu mpya wa kiuandishi katika kuzungumzia maswala mbalimbali yanayoikumba jamii. Nadharia ya usasaleo imeongoza utafiti huu katika uchanganuzi wakipengele cha urejeleomatini. Aina mbali mbali za matini zilizorejelewa katika uwasilishaji wa maudhui ya dhuluma zilitambulishwa na kufafanuliwa. Riwaya ya Msichana wa Mbalamwezi ilichaguliwa kimaksudi kwa kuwa inawasilishwa kwa simulizi nyingi fupi fupi zinazorejelea matini tofauti tofauti. Mbinu ya uchanganuzi wa yaliyomo mkabala wa kimaelezo ilitumika kuchanganua deta iliyohusiana na swala zima la urejeleomatini. Deta ilichanganuliwa kwa kuangazia maudhui, mandhari na mbinu za kiuandishi za kimajaribio. Matokeo yaliwasilishwa kwa njia ya kimaelezo. Ilibainika kuwa ukosefu wa utaratibu katika uendeshaji wa mambo ndiyo taswira kamili ya jamii ya sasa. Matini zilizorejelewa zimeonyesha kuwa mwananchi amedhulumiwa na kupewa huduma duni na viongozi. Makala hii imehakiki na kutathmini jinsi mwandishi anavyotumia mbinu ya urejeleomatini kama kunga ya uwasilishaji wa maudhui ya dhuluma katika riwaya ya Msichana wa Mbalamwezi.

Last modified: 2019-07-18 18:00:31