ResearchBib Share Your Research, Maximize Your Social Impacts
Sign for Notice Everyday Sign up >> Login

RIWAYA ZA KIMAJARIBIO BURUDANI AU KIKWAZO KWA MSOMAJI? MFANO WA RIWAYA TEULE ZA K.W. WAMITILA

Journal: International Journal of Advanced Research (Vol.10, No. 05)

Publication Date:

Authors : ;

Page : 468-478

Keywords : Riwaya Za Kisasa Riwaya Za Karne Ya 21 Muundo Mtindo Uandishi Bunifu Hadhira;

Source : Downloadexternal Find it from : Google Scholarexternal

Abstract

Makala hii imefafanua sababu za uchangamano wa muundo na mtindo wa riwaya za kisasa uliosababishwa na matumizi mapana ya mbinu za kimajaribio. Lengo mahususi lilikuwa kufafanua kuwepo kwa uandishi wa kimajaribio wenye kukanganya na athari zake kwa usomaji wa riwaya za kisasa. Japo kuna mitindo tofauti ya uandishi iliyozoeleka, mwandishi wa riwaya za kisasa hujikita katika ubunifu usiofuata mtindo mmoja maalum unaozifanya riwaya husika kuwa za kipekee. Makala hii imejibana katika ufafanuzi wa sababu za upekee wa riwaya hizo. Nadharia ya usasaleo imeuongoza mjadala huu katika ukusanyaji na uchanganuzi wa data. Mintarafu ya nadharia, mwandishi bunifu ana uhuru wa kuandika jinsi apendavyo bila kufuata utaratibu fulani mahususi. Mkabala wa uchanganuzi wa yaliyomo ulitumika kuchanganua data iliyohusiana na swala zima la ubunifu wa riwaya mpya ya Kiswahili. Data ilichanganuliwa kwa kuangazia maudhui na vipengele kadha vya mbinu za kiuandishi za kimajaribio. Riwaya za kisasa za Mwandishi, Msomaji na Mwandishi na Msichana wa Mbalamwezizimetumika kuangazia mchakato huu. Matokeo yamewasilishwa kwa njia ya maelezo. Riwaya zimebaini kuwa sura na ubunifu wa riwaya mpya ni zao la usomi. Kwa hivyo, ili kuelewa ujumbe katika riwaya za kisasa ni muhimu kwa msomaji kufanya utafiti wa kina na kuwa na ufahamu wa mambo mengi kiada ili kungamua yanayowasilishwa katika riwaya za kisasa.

Last modified: 2022-06-14 16:27:51