ResearchBib Share Your Research, Maximize Your Social Impacts
Sign for Notice Everyday Sign up >> Login

MIKAKATI YA KIMAZUNGUMZO KATIKA UUMBAJI WA UJINSIA MIONGONI MWA WAZULUFU NCHINI KENYA

Journal: International Journal of Advanced Research (Vol.8, No. 7)

Publication Date:

Authors : ; ;

Page : 1596-1605

Keywords : Wazulufu Ujinsia Utamaduni Mikakati Ya Kimazungumzo Utambulisho;

Source : Downloadexternal Find it from : Google Scholarexternal

Abstract

Utu uzima katika jamii nyingi za Kiafrika huhusishwa na uhuru wa kushiriki mahusiano anuwai ya kijamii. Utamaduni, matumizi ya lugha na miktadha ya kijamii huwa na nafasi muhimu katika kuelewa na kuthibiti mahusiano hayo. Licha ya uthibiti wa kijamii uliopo, mabadiliko ya kijamii (kiuchumi, kisiasa na kitamaduni) yamesababisha kuasiwa kwa tamaduni na kubadili mkondo wa mahusiano ya kijamii. Katika jitihada na ari ya kutafuta utambulisho na nafasi yao katika jamii, imetambuliwa idadi kubwa ya wazulufu hushiriki ngono za mapema. Lugha kama kipengele cha utambulisho ni muhimu katika kuelewa ulimwengu wa wazulufu. Makala haya ni uchanganuzi wa kiisimu wa uumbaji wa ujinsia kimazungumzo miongoni mwa wazulufu. Kupitia nadharia ya Uchanganuzi Hakiki wa Usemi hususan muundo msingi wa van Djik, makala haya yanatathmini mikakati mbali mbali ya kimazungumzo katika uumbaji wa ujinsia miongoni mwa wazulufu. Data ilikusanywa kupitia mijadala katika vikundi kiini. Kwa kutumia uchanganuzi wa yaliyomo, ilitambuliwa kuwa uumbaji wa ujinsia miongoni mwa wazulufu hutawaliwa na mikakati ya ukinai, urejelezi wa mamlaka, uainishaji, kitasfida, kisitiari, kitakwimu na kupiga chuku. Mikakati hii ya kimazungumzo hutumika kunyanyapaisha itikadi ya ubikira na kuhalalisha tabia za kujamiana miongoni mwa wazulufu.

Last modified: 2020-08-19 21:46:18